[sisilialaš]

sisilialaš
don jearat
makkárat min soagŋovierut
dološ jáhkut, sieiddit

in dieđe
ja heahpanan

jeara baicce
makkárat suopmelaččaid
vierut ja osku

de dieđán
ja heahpanan

© Inger-Mari Aikio
Iz: Roađđi – Rosa Boreal – Boreal Rose
Helsinki: Sivuvalo project, 2016
Avdio produkcija: Haus für Poesie, 2019

[Ewe, msisiliani]

Ewe, msisiliani
niulizeni
kuhusu mila zetu za ndoa
imani zetu za zamani
na madhabahu yetu ya kitamaduni

Siwachui
Na naona aibu

Afadhali mniulize
Kuhusu tamaduni za Ufini
Na imani zao

Nazifahamu hizo
Na naona aibu

Tafsiri: Christopher Okemwa & Ezra Nyakundi