L-ness

swahili

L-Ness

anglais

KUNA VILE

Utangamano ukiwa nguvu,
utengamano huwa ni undaifu,
Jifya moja tunajua haliinjiki chungu,
Mmoja atafuzu lakini
pamoja tutadumu,
Kukiwa kugumu, si sisi sugu,
Muhimu kumaliza
kile tulichoanzisha,
Kubainisha kati ya
ujenzi na mijengo,
Lengo na utengo,
kiasi cha kutimiza lengo,
chochote unachodo,
fanya mambo kizee,
mob ikimove na pseudopodia,
utasence kuna kitu
inaichocha na si sativa,
ni uyutman kusaka
uchumi bana,
any man asikuletee,
asikulete juu,
ju we ni woman,
na hauyuko ndani ya bar hapa,
we beba yako banner tena juu sana,
hadi misuli istunye
kama ya jiko pepetarer,
we ni hip hop labourer,
unadai nafasi kiveteran,
matamu na mathongo ,
ukiyaelewa u mwangazani,
aletaye maneno ndo yule ako gizani,
kuulizia ni ka
kumpigia mbuzi gitaa,
ona sasa wasee wamekuwa
vichaa machachari,
kila siku kwa habari ,
kuna balaa kiasi flani,
na hata wasee,
hawajajifunika kitalibani,
Chant down Babylon, hii ni vita flani,
baina ya good na evil,
toa O kwa the former inakuwa Sir God,
ukiongeza D kwa the latter,
inakuwa Devil,
si hivyo ndivyo ilivyo.

© L-Ness
Production audio: Literaturwerkstatt Berlin, 2015

THERE IS A WAY

Unity is strength,
disunity is weakness,
we know one finger can’t kill a louse,
one will get there but,
together we will succeed,
when shit is hard, we are hardcore,
it is important to finish,
what we started,
to differentiate between
development and buildings,,
an aim and derailment,
to the level of achieving an objective
whatever you do,
give it all your best,
when a lot of people move in masses,
you will sense there is something
motivating them and it is not sativa,
it is the youth in them as they search
for the better economy,
don’t let any man bring you down,
don’t let him harass you,
because you are woman,
and you are not in the bar here,
carry your banner higher and higher,
until your biceps harden,
like those ones of an oven fan blower
you are a hip hop laborer,
you are getting space like a veteran,
sweetness and bitterness,
you understand them in the light,
the bringer of chaos is in the dark,
asking for them is like
playing guitar to a goat,
look at guys now, they have become
dangerous hardheads,
everyday in the news,
there is some kind of disaster,
and those dudes,
are not even covered up like Talibans,
chant down Babylon, this is some war
between good and evil,
remove O from the former, its God,
add D to the latter,
it becomes Devil,
that is the way it is.

Translated by L-Ness