L-ness

swahili

 

KUNA VILE

Utangamano ukiwa nguvu,
utengamano huwa ni undaifu,
Jifya moja tunajua haliinjiki chungu,
Mmoja atafuzu lakini
pamoja tutadumu,
Kukiwa kugumu, si sisi sugu,
Muhimu kumaliza
kile tulichoanzisha,
Kubainisha kati ya
ujenzi na mijengo,
Lengo na utengo,
kiasi cha kutimiza lengo,
chochote unachodo,
fanya mambo kizee,
mob ikimove na pseudopodia,
utasence kuna kitu
inaichocha na si sativa,
ni uyutman kusaka
uchumi bana,
any man asikuletee,
asikulete juu,
ju we ni woman,
na hauyuko ndani ya bar hapa,
we beba yako banner tena juu sana,
hadi misuli istunye
kama ya jiko pepetarer,
we ni hip hop labourer,
unadai nafasi kiveteran,
matamu na mathongo ,
ukiyaelewa u mwangazani,
aletaye maneno ndo yule ako gizani,
kuulizia ni ka
kumpigia mbuzi gitaa,
ona sasa wasee wamekuwa
vichaa machachari,
kila siku kwa habari ,
kuna balaa kiasi flani,
na hata wasee,
hawajajifunika kitalibani,
Chant down Babylon, hii ni vita flani,
baina ya good na evil,
toa O kwa the former inakuwa Sir God,
ukiongeza D kwa the latter,
inakuwa Devil,
si hivyo ndivyo ilivyo.

© L-Ness
Producción de Audio: Literaturwerkstatt Berlin, 2015