L-ness

swahili

 

IMANI YAKO

Kila mtu anataka sehemu mwangazani,
Kwa imani kila usiku ina mchana,
Mashinani gizani
hawakutoss tequila,
Walicross kwa teke na ila,
Kwa imani hatutaki uongizi wa kiimla,
Kila kukikucha nakariri
mashairi toka kichwani,
Imani yako iziguard zako toes,
Wadosi wamekuwa shavu dodo,
Yutman anacomplain
juu ya low wage,
No way wanaeza explain,
tunalipa tax over.
Nikiflow kwa hii pen
ka fountain we know,
Visivyo huwa ndivyo,
Ni kwa imani
Milima ilisonga,
milango ya gereza ikafunguka,
Mkumbuke sila na paulo,
Mi sikufundishi, mi nakubariki,
Kiwiliwili ki yadi na fikira mbali,
Chochote ufanyacho ni juu yako,
Popote upitapo ni bidii yako,
Gaa gaa na upwa usile wali mkavu,
Mbachao upo msala upitao.
Ehe, kama kawa, ni imani yako,
So wachana na pride, greed, envy,
Wrath, sloth, ongezea lust na gluttony,
Basic temptations huleta tension,
Mc namove motion ya imani,
Mp anakandamiza tumaini,
Tunaamini tumajiarmy kwa army,
Ka injili na G3 not forgetting to mention,
Neno ndo ammunition.

© L-Ness
Audio production: Literaturwerkstatt Berlin, 2015