L-ness

swahili

 

HAKUNA MTU

Vipraco, art ya, social control,
Sociology ya poverty,
na psychology ya the ghetto,
G ako hustle, lakini,
F the five o,
KiKavuludi sharudi police reforms,
Vifo extrajudicial zifike kikomo,
Ashindwe rider wa the
red horse revelations,
Kaboom hakuna mtu
ni hu dem akikam through,
Ni ma fire in the hole!
Hakuna mtu anaconsole
muthii ako parole,
anasisitiza ukweli maishani,
haki street,
na maendeleo gishagi,
hakuna mtu ni mtemi katika kipaza,
hakuna mtu anataka kusimama,
pia hakuna mtu anadai
usawa na raha bila karaha,
ulimwenguni,
ndo kukiulizwa ni nani ako fere
kilinani kuadvocatia ukweli?
Hakuna mtu anajitolea bila kwere,
Kila mtu anapotelea,
hakuna mtu anatokea na kukemea
Injustice kwa society na
brutality ya ma five o,
Especially kwa wale
ma sheikh wa pwani,
Za kumwagia mse acid
kichwani ndo gani?
Hakuna mtu anaweza kukushika
hata ka umagandiza na kubangaiza,
Vina vikiganda skioni
mfano wa gundi.

© L-Ness
Audio production: Literaturwerkstatt Berlin, 2015