L-ness

swahili

 

HIP HOP HALISI

Nimechoose maneno ya kukuconfuse,
Ndani ya ubeti kukulose,
Ndo niko used to,
Full kueneza upendo kwote,
Kiupepo napita sehemu zote,
Sisare kivuli,
Echo imeshaskika toka Soweto,
Mchezo ni on your marks,
Get set, imesikika shot,
Nimekumake ulook,
Hapa hivi bila aibu,
Bila kuwatch out for
Misumaa inasinzia mchana kutwa,
Zisipoeducate,
watafunzwa na ulimwengu,
Ambapo kipofu anasikia
usichokiona,
Na kiziwi anaona,
usichokisikia,
Sasa, inakuwaje?
Sisi tulishatafsiri,
tukafanya mambo,
Na still kiDre chronically
kwenya mic
kuna jambo
mbiu ni ya mgambo,
imebaki kila time ni wakati
wa kuweka senti kwenye beti,
zijaze benki, sura ikiwa,
ni ya kuchora ukutani,
kwa graffiti.

© L-Ness
Audio production: Literaturwerkstatt Berlin, 2015